iqna

IQNA

IQNA--Mnamo mwaka 1979, mara tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa siku ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, akiwa amesimama imara katika kupigania haki za watu wote wanaodhulumiwa ulimwenguni.
Habari ID: 3480457    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28

IQNA-Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480454    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema maandamano ya kimataifa ya Siku ya Quds, Ijumaa hii, "kwa msaada wa  Mwenyezi Mungu, yatakuwa moja ya maandamano bora, ya kupendeza zaidi, na yenye heshima zaidi."
Habari ID: 3480449    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28

IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa wananchi wa Iran kuonyesha umoja na mshikamano wao wakati wa Siku ya Kimataifa ya Quds, akisisitiza kwamba kujitokeza kwa wingi wananchi katika siku hii kutaonyesha msaada usiotetereka wa Jamhuri ya Kiislamu kwa malengo ya ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3480446    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/27

IQNA – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina, Hamas, imetoa wito wa maandamano duniani kote wiki hii kwa ajili ya kuwasaidia na kufungamana na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, mji mtakatifu wa al-Quds na Msikiti wa al-Aqsa. Katika Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3480442    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/26

IQNA – Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) imetayarisha bango la Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu wa 1446 H sawa na 2025.
Habari ID: 3480437    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/25

IQNA – Siku ya Kimataifa ya Quds ni fursa ya kuonyesha msaada wa umma kwa  taifa la Palestina na ukombozi wa al-Quds, amesema afisa mwandamizi nchini Iran.
Habari ID: 3480435    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/25

Kadhia ya Palestina
IQNA-Mkuu wa Makao Makuu ya Intifada na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran, Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, amesisitiza umuhimu wa kupanga na kufanya juhudi za kufanikisha maandamano makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu.
Habari ID: 3480232    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/18

Siku ya Quds
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mhimili wa muqawama una uhakika wa kupata "ushindi mkubwa" katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3478636    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/06

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran
IQNA- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa Tehran ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina na kusema: "Utawala bandia wa Kizayuni unaoua watoto sasa umebadilika na kuwa nembo ya jinai katika mfumo wa kisheria wa kimataifa.
Habari ID: 3478635    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Quds
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) anasema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika hivi karibuni, akibainisha kuwa Marekani inaiunga mkono waziwazi Israel.
Habari ID: 3478634    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Quds
IQNA-Mamillioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo yamefanyika leo katika miji na maeneo mbalimbali nchini Iran.
Habari ID: 3478633    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Kimataifa ya Quds
IQNA-Siku ya Quds mwaka huu 2024 imewadia huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiwa umekwama kwenye kinamasi cha Gaza licha ya mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya katika eneo hilo la Palestina ambayo tokea Oktoba mwaka jana hadi sasa yamepelekea Wapalestina wasiopungua 33,000 kuuawa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
Habari ID: 3478632    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05

Siku ya Quds
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema siku ya Quds mwaka huu itakuwa uasi wa kimataifa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na kuongeza kuwa: "Utawala wa Kizayuni wa Israel utazabwa kibao usoni kutokana na shambulio lake dhidi ya majengo ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, mapema wiki hii."
Habari ID: 3478630    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04

Kadhia ya Palestina
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, na kwamba operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imemweka adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti.
Habari ID: 3478629    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04

Siku ya Quds
IQNA - Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hasan Nasrallah ametoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi barabarani Ijumaa ijayo ambayo inaadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3478605    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Imam wa Sala ya Ijumaa wa ya Tehran amesema kwamba wananchi wa Iran walichukua hatua madhubuti na kubwa kuelekea katika kuliwezesha zaidi taifa katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, na ametoa shukrani zake kwa ushiriki mkubwa wa wananchi katika maandamano ya siku hiyo ya kuwaunga mkono mapambano ya ukombozi ya Wapalestina.
Habari ID: 3476927    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/28

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: "kuhudhuria kwa hamasa kubwa wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Quds Duniani bila shaka kumeyafanya maandamano ya mwaka huu kuwa moja ya maandamano yenye msisimko na taathira kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni na kuwapa faraja Mujahidina wanaopambana katika njia ya ukombozi wa Quds."
Habari ID: 3476876    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/16

Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kutaka kuweko harakati ya kimataifa ili kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kuhitimisha uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
Habari ID: 3476867    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14

Azimio la Siku ya Kimataifa ya Quds
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran walioshiriki katika maandamano ya leo ya Siku ya Kimataifa ya Quds wametangaza kuwa Umoja ndio ufunguo wa kushinda njama za ubeberu wa kimataifa.
Habari ID: 3476865    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14